Chama cha Wauguzi Tanzania
(TANNA) kimesema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya video iliyosambaa
kwenye mitandao ya kijamii tarehe 05 January 2023, na kuzua taharuki kwa jamii
ikiwahusisha Watumishi wa Kada ya Afya wawili ambao ni Rose Shirima (Muuguzi
Mkunga) na James Getogo Chuchu (Mtekenolojia wa maabara), wote wakitokea
Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Zahanati ya Ishihimulwa Mkoani Tabora.
Kufuatia tuhuma hizo Chama hicho
kwa kushirikiana na Viongozi wa tawi la Tabora walifanya uchunguzi ili
kujiridhisha na uhalisia wa tukio hilo ambapo Chama kimewatoa hofu Wananchi
hasa wanaopata huduma za afya katika Zahanati hiyo kuwa hakuna vitendanishi
vyovyote vilivyoisha muda wake ambavyo vilikuwa vinatumika katika kituo hicho
kama ilivyokuwa inaelezwa na Mtekinolojia wa Maabara katika video iliyosambaa
na hata kusababisha taharuki nchini.
“Vitendanishi vilivyopo
vinakaribia kuisha muda wake yaani bado vina miezi 3 mbele mpaka tarehe
14.04.2023, hivyo alichokuwa anasimamia Muuguzi (Rose) kilikuwa sahihi kwa
kufuata utaratibu wa mfumo wa udhibiti bidhaa (Stock control system using FIFO
and FEFO principles), lakini pia alikuwa akisimamia maamuzi ya kikao chao cha
ndani”