Winga machachari wa Simba Shiza kichuya ameibuka na kumuomba radhi babayake mzazi baada ya kuisawazishia timu yake ya simba bao pekee katika dakika za lala salama siku ya tarehe 01/10/2016
na timu ya Yanga katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Akihojiwa na Televisheni ya ITV katika kipindi cha michezo Shiza amesema imempasa kutumia muda huu kumuomba radhi baba yake mzazi kutokana kuwa na mapenzi makubwa na timu ya Yanga hivyo kitendo cha yeye kuisawazishia timu yake goli anajua kilimkera sana Babayake mzazi,
Kichuya ndiye aliye isawazishia timu ya simba goli dakika tatu kabla ya mpira kumalizika goli lililopatikana kwanjia ya kona iliyo tinga mojakwa moja nyavuni baada ya kupigwa na mchezaji huyo katika mahojiano na mwandishi wa habari kichuya alidai kuwa hakuna kitu kilichokuwa kikimuuma hasa baada ya kujikuta wapo pungufu kimchezo siku hiyo na tayari walikuwa wameshafungwa goli moja na dakika nazo ndio zilikua zinayoyoma na kila akiwatazama viongozi wake pamoja na mashabiki wa Simba alibaini kuwa hawana furaha,Kitendo hicho kilimfanya acheze mpira kwa kujituma kuhakikicha timu yake haipotezi mchezo huo na mara baada ya timu yake kupata kona katika dakika za lala salama alijitolea kupiga kona hiyo huku akiomba mungu lengo lake litimie na alimshukuru mungu sana baada ya kuisawazishia timu yake goli hilo kwani katika malengo yake ya soka kichuya alidai kuwa alikua na ndoto ya kuichezea timu ya Simba.
0 comments:
Post a Comment