Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka 1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana, na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na chuma kama majembe,mapanga, visu, silaha kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano Wachaga,na wamekuwa na uhusiano tangu siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa Wasambaa (Washambaa).
SEHEMU YA PILI
Jamii za Wapare zimegawanyika katika makundi ya Wafugaji na Wakulima. Wakati Wafugaji wengi walihamia katika tambarare za Upareni, Wakulima wao waliishi milimani na wafuaji wa vyuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na uwezekano wa kupata chuma. Kwa asili Wapare hupeleka vijana wakiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia,japo siku hizi tamaduni za kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache. Hata hivyo wapare wa Mwanga wamegawanyika katika jamii mbili: Wasangi na Wagweno. Wakati wasangi wanaongea kipare kinachoongelewa pia na Wapare wa maeneo mengine, Wagweno wao wana lugha yao iitwayo Kigweno. Kigweno ni mchanganyika wa Kipare na Kichagga. Hii inaonesha kuwa asili ya Wagweno ni uchagani japo zipo nadharia kadha wa kadha zinazoeleza asili ya wagweno kuwa huenda hata hawana asili ya uchaga wala upare lakini mbali na uhusiano wa lugha kinachofanya waonekane kuwa ni sehemu ya wapare ni namna tamaduni zao nyingine zinavyofanana na wapare,pia kuchanganyika katika maisha ya kila siku kwenye milima ya wapare pamoja na wagweno wengine kuwa na majina ya koo zinazofanana na za wapare kama Wasuya na Wavungi. Hata hivyo mila na desturi nyingi za Wagweno zinafanana zaidi na zile za wapare wengine.
Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na biashara, ndio maana hata leo wana uchumi mzuri katika viwango vya Tanzania. Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti,kwa kila koo na eneo lao la tambiko, katika karne ya 19 hadi 20 wamisionari waliingia maeneo mengi ya Upare.
Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana kutokana na maeneo, walio Kusini mwa wilaya ya Same katika maeneo ya Ndungu,Kihurio,Bendera,Hedaru, Makanya,Suji,Chome,Tae,Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisa la Sabato wengi sana,maeneo kama Chome,Mbaga,Gonja, Vudee yana waumini wengi wa kanisaa la Kilutheri, Katika Wilaya ya Mwanga kuna idadi kubwa ya Walutheri na Waislamu. Wakatoliki, japo ni wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara juu, Vumari, na Mbaga.
Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile hata majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila kama vile Wasambaa na Wanguu. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.
USIKOSE SEHEMU YA TATU..........
0 comments:
Post a Comment