Wafanyakazi wa Kampuni ya Usafiri ya Jijini Dar es salaam UDART kitengo cha Usafi na Uhudumu wa Vituo vya Mabasi ya Mwendo wa haraka wamegoma kufanya kazi wakiushinikiza Uongozi wa Kampuni hiyo kuwalipa madai ya mishahara ya miezi miwili ambayo wanadai kutolipwa.
Wafanyakazi hao waliokutwa na Camera za Channel Ten nje ya Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo eneo la Jangwani jijini Dar es salaam wamelalamikia kitendo cha Kampuni hiyo kutowalipa mishahara pamoja na posho na kusababisha wakabiliwe na maisha magumu huku wengine wakishindwa kuhudumia familia zao na kulipa kodi za nyumba.
Wamedai kuwa licha ya kuwasilisha malalamiko yao katika uongozi wa juu wa kampuni hiyo, hakuna hatua zilizochukuliwa na badala yake wamekuwa wakitishwa kufukuzwa kazi bila malipo yoyote, hivyo wameiomba Serikali kuingilia kati ili wapate stahiki zao.
Baada ya kilio hicho Channel Ten ilibisha Hodi katika Ofisi za kampuni hiyo na kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa UDART David Mgwasa ambaye alikiri kuwepo Mgomo huo:
0 comments:
Post a Comment