Thursday, July 28, 2016

Historia ya Kabila la Wapare Sehemu ya 3




Ilipo ishia wiki iliyo pita...

Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile hata majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila kama vile Wasambaa na Wanguu. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.

Endelea..
Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga mana yake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa watu wa makabila haya wote walitokea Kenya. Wachagga walitangulia wakawahi kuishi maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima Kilimanjaro. Wapare walikuja baadae na walipotaka kuishi na wachagga ndipo vita ikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu ikiwa na maana ya "vareasa" au watu wanaotumia mishale
   Wapare wana koo nyingi na majina mengi yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au mazingira ya kuzaliwa kwao,mfano Mbwambo,Mjema,Msangi,Mgweno,Mvungi,Msuya,Mgonja n.k, wana asili ya maeneo yao.

Mifano ya majina ya watoto wa kipare
  Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)
Ingiahedi, Itikija, Kafue,Kapingu, Kapwete, Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho, Kondisha,Ludao, Mchikirwa, Mshinwa, Naanjela, Nacharo, Naelijwa, Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete, Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa,Namkunda,Nabera,Namangi,Nangasu,Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu, Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji, Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza, Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero, Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri, Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe, Nietiwe, Ntevona, Sangiwa,Shode, Yunesi.

   Majina ya kiume:
Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema, Chedieli,Chuma, Elieseri, Eliesikia,Elinighenja,Elibariki,Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni, Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio, Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo, Kalinga (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa),Kalutu, Kambaita (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni, Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiangi, Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho (Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe, Kileng'a, Kinenekejo (Wengine hufupisha na kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo, Hayo ni baadhi ya majina ya kiume Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza akachukua au akamwita mtoto wake. Pia majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi ya Wapare yakiwa na maana tofauti tofauti.

 
      Tamaduni,mila na desturi za wapare zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu zote.Hapo kale wapare pia waliweza kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli za jadi jambo ambalo wapo baadhi ya wapare ambao mpaka leo wanaweza.Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga maarufuku utawala wa jadi.Kiongozi huyu aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.Pia walikuwepo hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua eneo hilo.Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea kama siyo kuisha kabisa.Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalum kama kwenye jando au unyago,pia nyimbo za kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na sherehe nyingine na kupendezesha tukio husika.Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali,hadithi,maigizo n.k wakati wa mapumziko na matukio fulani.Hali hii ilisababisha kuwepo wasanii wengi maarufu wa maigizo na nyimbo kama Halima madiwa Jacob Steven(JB),Sinta,Sara Mvungi,Roma Mkatoliki na wengine wengi.
Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi wapare walikuwa wakiamini tiba za mitishamba kwa kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu,kirutu n.k ipo miti maarufu kama mwori ambayo ilitumika.Mchango wa dawa za mitishamba kwa watoto na watu wazima ulionesha mafanikio tangu zamani na hata sasa.

  Michezo ya utotoni ni moja ya mambo ambayo yalikua yakiimarisha tamaduni za kipare baadhi ya michezo  ni kama Kajanja .Mchezo wa kujificha uliokuwa ukijulikana kama Kibe

Usikose sehemu ya 4

0 comments:

Post a Comment