Ligi kuu ya vodacom imeendelea leo hii katika uwanja
wa taifa kati ya wenyeji Simba sc dhini ya mbao fc toka jijini mwanza mchezo
ambao ulikuwa ni kiporo kwa timu hizo kukamilisha mzunguko wa 19 mchezo ambao
umeanza majira ya 16:00hrs kwa timu zote kushambuliana kwa kasi huku mbao
wakionyesha kukamia zaidi mchezo huo na kadri muda ulivyozidi koyoyoma simba
walionekana kuanza kusakata kabumbu huku wakilisakama lango la mbao kwa kasi
zaidi na dakika ya 37 Shiza kichuya alifungua ukurasa mpya kwa kuiyandikia
simba goli la kwanza baada ya kupokea pasi toka kwa Emanuel okwi na dakika tatu
badae Emanueli Okwi aliiyandikia simba goli ta pili kwa mkwaju wa penati baada
ya kuchezewa vibaya akiwa ndani ya kumi na nane na mpaka mapumziko Simba mbili
mbao sifuri.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi zaidi kwa timu ya simba kucheza kwa kuonana kitendo
kilicho wafanya wachezaji wa mbao kupoteana huku wakihaha kutafuta mpira na
dakika ya 70 Emanuel okwi aliiyandikia simba bao la tatu baada ya kupokea pasi
safi toka kwa mzamiru yasini. Mvua ya magoli iliendelea kulinyeshea lango la
mbao na mpaka mwisho wa mchezo mbao walijikuta wakibamizwa goli tano kwa bila
magoli yaliofungwa na Erasto nyoni dakika ya 82 pamoja na Nicolous Gyan dakika
ya 86. kipigo hichi huenda kimetokana na baadhi ya kauli za kocha wa mbao wakati alipokuwa akihojiwa juu ya umuhimu wa mchezo huo kwake na kudai kuwa hana presha yoyote juu ya mchezo huo kwani Simba ni timu ya kawaida sana kwake.
0 comments:
Post a Comment