Tuesday, June 28, 2016

YANGA YASHINDWA KUTUMIA VYEMA UWANJA WA NYUMBANI

Yanga yakubali kishapo cha goli moja kwa bila nyumbani

Mkuu wa mkoa Dsm Paul Makonda amemsimamisha kazi Msimamizi mkuu wa barabara


Mkuu wa mkoa Dsm Paul Makonda amemsimamisha kazi Msimamizi mkuu wa barabara katika mkoa wa dsm Injinia Josephat Shehemba kutokana na barabara nyingi katika jiji la dsm kujengwa chini ya viwango,kushindwa kusimamia wakaguzi wa ubora wa viwango na kushindwa kutimiza wajibu wake kikazi.
Sambasamba na kusimamishwa huko Vyombo vya Uchunguzi ikiwemo takukuru wamepewa jukumu la kumchunguza pamoja na kuchunguza makampuni ya Ukandarasi yaliyopewa jukumu la ujenzi na kujenga chini ya Viwango,ujenzi wa muda mrefu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.
Aidha Bw,Makonda amewaonya watumishi wote wa mkoa wa dsm kuhakikisha wanatimiza majukumu yao waliyopewa na kuonya kuwa hata sita kuchukua hatua kali kwa mtumishi yeyote wa mkoa iwapo hatawajibika katika kitengo au idara yake aliyopangiwa.
Chanzo chanel ten

Sweeden imefungua Barabara ya Umeme(eHighway) kwa magari Makubwa!


Pengine Sweeden ndio inaweza ikawa nchi ya kwanza kuja na teknolojia hii kwa magari makubwa.Magari haya yanatembea katika barabara ambazo zimeunganishwa na nyaya za umeme. Kilicho fanyika ni kwamba magari hayo kwa juu yameunganishwa na nyaya ambazo zinaelea (zilizo shikiliwa na nguzo) Jina la barabara hiyo ni eHighway
   Magari ambayo yanapita katika barabara hiyo ni yale makubwa kabisa inasemekana wakati magarihayo yakiwa katika barabara hiyo yatakua hayatumii mafuta  lakini yakitoka nje ya barabara hiyo ya umeme ndiyo yatakuwa yanatumia mafuta kama kawaida

Na mwandishi wetu



Roy Hodgson amejiuzuluzu kama kocha mkuu wa England baada ya kikosi chake kuchezea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Iceland kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.Kocha huyo mwenye miaka 68 amekinoa kikosi cha England kwa miaka minne akichukua nafasi ya kocha raia wa Italy Fabio Capello lakini amejikuta akishinda mechi tatu pekee kwenye mashindano makubwa ya kimataifa.
Iceland taifa lenye wakazi wasiopungua 330,000 ilikuwa ndiyo timu inayopewa nafasi ndogo zaidi kwenye michuano Ulaya inayoendelea Ufaransa.
“Samahani, inabidi nimalize kwa style hii lakini tayari yaliyotokea yametokea,” amesema Hodgson.
“Natumaini bado mtaendelea kuiona timu ya England kwenye fainali za mashindano makubwa hivi karibuni”, aliongeza.
“Kwa sasa ni wakati wa mtu mwingine kuja kuendelea na vijana wenye njaa na wenye vipaji.”
Hodgson ambaye ameshinda mechi 33 kati ya 56 akiwa madarakani, anagekuwa nje ya mkataba baada ya kumalizika kwa mashondano haya na inataarifa angeweza kuongezwa mkataba mwingeine baada ya kufanya mazungumzo na ma-boss wa FA.
Mwenyekiti wa FA Greg Dyke alishatoa kauli kwamba, Hodgson angeonezewa mkataba wake kama tu timu ingefanya vizuri Ufaransa, huku akisema angalau hatua ya robo fainali lakini walitakiwa kuifunga Iceland ili kufanikisha hilo.
Kauli iliyotolewa na FA baada ya Hodgson kujiuzulu, FA imesema: kama taifa
England ilifuzu kucheza Euro 2016 kwa rekodi ya aina yake. Walianza michuano hiyo kwa sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Russia kabla ya kuichapa Wales 2-1 na kutoka sare ya 0-0 Slovakia kwenye hatua ya makundi na kufanikiwa kufuzu kwa hatua ya 16 bora.
Chini ya Hodgson kikosi cha England, walifika hatua ya robo fainali kabla ya kuchezea kichapo na Italykwenye michuano ya Ulaya iliyopita .

KILICHOANDIKWA NA MAGAZETI KATIKA KURASA ZA MICHEZO LEO JUMANNE

Mpenda soka mwenzangu, nimekuwekea kilichojiri kwenye magazeti ya Tanzania kwa upande wa habari za Michezo. 



















Sunday, June 26, 2016

Lionel Messi: Argentina forward retires from international football

Argentina and Barcelona forward Lionel Messi retired from international duty after missing in a penalty shootout as Chile won the Copa America final.
"For me the national team is over. I've done all I can, it hurts not to be a champion," the 29-year-old said.
With Barcelona, Messi has won eight La Liga titles and four Champions Leagues.
But his only major international honour is 2008 Olympic gold, with Argentina now having lost three major finals in three years.
Argentina were beaten 1-0 in the 2014 World Cup final by Germany before two Copa America final defeats by Chile on penalties. He was also on the losing side against Brazil in the 2007 Copa America final.
After Sunday's match finished 0-0 in 120 minutes, Chile won 4-2 on penalties.
Messi's penalty miss was Argentina's first attempt in the shootout and it ballooned over the bar after Sergio Romero had denied Chile's Arturo Vidal.
Lucas Biglia also missed from 12 yards, with Chilean substitute Francisco Silva scoring the decisive spot-kick in the final in East Rutherford, New Jersey.

 

 

 


Na Mwandishi wetu


KATIBU MPYA WA SIMBA AMEAHIDI MAMBO MAKUU MAWILI KWA MASHABIKI

Patrick Kahemele amesaini mkata wa miaka miwili kuitumikia Simba kama Katibu Mkuu wa klabu hiyo baada ya mabingwa hao wa zamani kukaa kwa muda mfefu bila kuwa na mtendaji mkuu wa shughuli za klabu yao.
Kahemele ameahidi mambo makuu mawili katika uongozi wake wa miaka miwili ndani ya Simba. Jambo la kubwa na kwanza ni kuifanya Simba ijitegemee na kuacha kutegemea mifuko ya watu wachache lakini huu ukiwa ni mpango wa muda mrefu. Jambo la pili ni kuisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ilioukosa kwa misimu minne sasa.
“Simba ni timu kubwa, imekuwa na hamu ya mafanikio ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Tukizungumza nje ya uwanja, klabu inahitaji kujitegemea na naamini wana Simba wana mawazo mengi, kikubwa ni kukaa na kushirikiana tuweke mawazo yetu pamoja na kuona ni jinsi gani tunaweza tukaikwamua klabu ya Simba kutoka kutegemea mifuko ya watu wachache hadi kuwa klabu inayojitegemea na kusimama yenyewe,” amesema Kahemele ambaye ataanza majukumu yake ya kazi Julai 1 mwaka huu.
“Hiyo ni mipango ya muda mrefu katika kipindi cha miaka miwili ningependa nifanikishe hilo ambalo hata nikiondoka mimi pamoja na viongozi wenzangu tunakuwa tumefanya kitiu flani. Lakini la msingi kabisa ni kuhakikisha msimu ujao lazima ubingwa uende Msimbazi kwasababu Simba ni timu ambayo imezoea kushinda vikombe lakini kazi hiyo inaanzia kwenye usajili, lazima tuwe na timu nzuri, benchi la ufundi zuri, timu ipate kambi na huduma nzuri na vyote hivyo vikiwekwa pamoja hakuna linaloshindikana.”
Anatoa neno kuhusu mashabiki wa ‘mnyama’
“Mashabiki wa Simba ni wastaarabu sana, sijawahi kuona mashabiki wa Simba wakitia presha, mashabiki wa Simba wakikupa shida ujue umewakosea lakini kama hujawakosea hawana shida kabisa.”

                                            

RAIS MAGUFULI AMETEUA WAKUU WA WILAYA 139 NA KUPANGUA BAADHI YA WAKUU WA MIKOA
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
1. Arusha - Mrisho Mashaka Gambo
2. Arumeru - Alexander Pastory Mnyeti
3. Ngorongoro - Rashid Mfaume Taka
4. Longido - Daniel Geofrey Chongolo
5. Monduli - Idd Hassan Kimanta
6. Karatu - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
1. Kinondoni - Ally Hapi
2. Ilala - Sophia Mjema
3. Temeke - Felix Jackson Lyaviva
4. Kigamboni - Hashim Shaibu Mgandilwa
5. Ubungo - Hamphrey Polepole
DODOMA
1. Chamwino - Vumilia Justine Nyamoga
2. Dodoma - Christina Solomon Mndeme
3. Chemba - Simon Ezekiel Odunga
4. Kondoa - Sezeria Veneranda Makutta
5. Bahi - Elizabeth Simon
6. Mpwapwa - Jabir Mussa Shekimweli
7. Kongwa - John Ernest Palingo
GEITA
1. Bukombe - Josephat Maganga
2. Mbogwe - Matha John Mkupasi
3. Nyang'wale- Hamim Buzohera Gwiyama
4. Geita - Herman C. Kipufi
5. Chato - Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
1. Mufindi - Jamhuri David William
2. Kilolo - Asia Juma Abdallah
3. Iringa - Richard Kasesela
KAGERA
1. Biharamulo- Saada Abraham Mallunde
2. Karagwe - Geofrey Muheluka Ayoub
3. Muleba - Richard Henry Ruyango
4. Kyerwa - Col. Shaban Ilangu Lissu
5. Bukoba - Deodatus Lucas Kinawilo
6. Ngara - Lt. Col. Michael M. Mtenjele
7. Missenyi - Lt. Col Denis F. Mwila
KATAVI
1. Mlele - Rachiel Stephano Kasanda
2. Mpanda - Lilian Charles Matinga
3. Tanganyika- Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA
1. Kigoma - Samsoni Renard Anga
2. Kasulu - Col. Martin Elia Mkisi
3. Kakonko - Col. Hosea Malonda Ndagala
4. Uvinza - Mwanamvua Hoza Mlindoko
5. Buhigwe - Col. Elisha Marco Gagisti
6. Kibondo - Luis Peter Bura
KILIMANJARO
1. Siha - Onesmo Buswelu
2. Moshi - Kippi Warioba
3. Mwanga - Aaron Yeseya Mmbago
4. Rombo - Fatma Hassan Toufiq
5. Hai - Gelasius Byakanwa
6. Same - Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI
1. Nachingwea- Rukia Akhibu Muwango
2. Ruangwa - Joseph Joseph Mkirikiti
3. Liwale - Sarah Vicent Chiwamba
4. Lindi - Shaibu Issa Ndemanga
5. Kilwa - Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA
1. Babati - Raymond H. Mushi
2. Mbulu - Chelestion Simba M. Mofungu
3. Hanang' - Sara Msafiri Ally
4. Kiteto - Tumaini Benson Magessa
5. Simanjiro - Zephania Adriano Chaula
MARA
1. Rorya - Simon K. Chacha
2. Serengeti - Emile Yotham Ntakamulenga
3. Bunda - Lydia Simeon Bupilipili
4. Butiama - Anarose Nyamubi
5. Tarime - Glodious Benard Luoga
6. Musoma - Dkt. Vicent Anney Naano
MBEYA
1. Chunya - Rehema Manase Madusa
2. Kyela - Claudia Undalusyege Kitta
3. Mbeya - William Ntinika Paul
4. Rungwe - Chalya Julius Nyangidu
5. Mbarali - Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO
1. Gairo - Siriel Shaid Mchembe
2. Kilombero - James Mugendi Ihunyo
3. Mvomero - Mohamed Mussa Utali
4. Morogoro - Regina Reginald Chonjo
5. Ulanga - Kassema Jacob Joseph
6. Kilosa - Adam Idd Mgoyi
7. Malinyi - Majula Mateko Kasika
MTWARA
1. Newala - Aziza Ally Mangosongo
2. Nanyumbu - Joakim Wangabo
3. Mtwara - Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
4. Masasi - Seleman Mzee Seleman
5. Tandahimba- Sebastian M. Walyuba
MWANZA
1. Ilemela - Dkt. Leonald Moses Massale
2. Kwimba - Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
3. Sengerema- Emmanuel Enock Kipole
4. Nyamagana- Mary Tesha Onesmo
5. Magu - Hadija Rashid Nyembo
6. Ukerewe - Estomihn Fransis Chang'ah
7. Misungwi - Juma Sweda
NJOMBE
1. Njombe - Ruth Blasio Msafiri
2. Ludewa - Andrea Axwesso Tsere
3. Wanging'ombe- Ally Mohamed Kassige
4. Makete - Veronica Kessy
PWANI
1. Bagamoyo - Alhaji Majid Hemed Mwanga
2. Mkuranga - Filberto H. Sanga
3. Rufiji - Juma Abdallah Njwayo
4. Mafia - Shaibu Ahamed Nunduma
5. Kibaha - Asumpter Nsunju Mshama
6. Kisarawe - Happyness Seneda William
7. Kibiti - Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA
1. Sumbawanga - Dkt. Khalfan Boniface Haule
2. Nkasi - Said Mohamed Mtanda
3. Kalambo - Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA
1. Namtumbo - Luckness Adrian Amlima
2. Mbinga - Cosmas Nyano Nshenye
3. Nyasa - Isabera Octava Chilumba
4. Tunduru - Juma Homela
5. Songea - Polet Kamando Mgema
SHINYANGA
1. Kishapu - Nyambonga Daudi Taraba
2. Kahama - Fadhili Nkulu
3. Shinyanga - Josephine Rabby Matiro
SIMIYU
1. Busega - Tano Seif Mwera
2. Maswa - Sefu Abdallah Shekalaghe
3. Bariadi - Festo Sheimu Kiswaga
4. Meatu - Joseph Elieza Chilongani
5. Itilima - Benson Salehe Kilangi
SINGIDA
1. Mkalama - Jackson Jonas Masako
2. Manyoni - Mwembe Idephonce Geofrey
3. Singida - Elias Choro John Tarimo
4. Ikungi - Fikiri Avias Said
5. Iramba - Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE
1. Songwe - Samwel Jeremiah
2. Ileje - Joseph Modest Mkude
3. Mbozi - Ally Masoud Maswanya
4. Momba - Juma Said Irando
TABORA
1. Nzega - Geofrey William Ngudula
2. Kaliua - Busalama Abel Yeji
3. Igunga - Mwaipopo John Gabriel
4. Sikonge - Peres Boniphace Magiri
5. Tabora - Queen Mwashinga Mlozi
6. Urambo - Angelina John Kwingwa
7. Uyui - Gabriel Simon Mnyele
TANGA
1. Tanga - Thobias Mwilapwa
2. Muheza - Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
3. Mkinga - Yona Lucas Maki
4. Pangani - Zainab Abdallah Issa
5. Handeni - Godwin Crydon Gondwe
6. Korogwe - Robert Gabriel
7. Kilindi - Sauda Salum Mtondoo
8. Lushoto - Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
1. Arusha - Mrisho Mashaka Gambo
2. Arumeru - Alexander Pastory Mnyeti
3. Ngorongoro - Rashid Mfaume Taka
4. Longido - Daniel Geofrey Chongolo
5. Monduli - Idd Hassan Kimanta
6. Karatu - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
1. Kinondoni - Ally Hapi
2. Ilala - Sophia Mjema
3. Temeke - Felix Jackson Lyaviva
4. Kigamboni - Hashim Shaibu Mgandilwa
5. Ubungo - Hamphrey Polepole
DODOMA
1. Chamwino - Vumilia Justine Nyamoga
2. Dodoma - Christina Solomon Mndeme
3. Chemba - Simon Ezekiel Odunga
4. Kondoa - Sezeria Veneranda Makutta
5. Bahi - Elizabeth Simon
6. Mpwapwa - Jabir Mussa Shekimweli
7. Kongwa - John Ernest Palingo
GEITA
1. Bukombe - Josephat Maganga
2. Mbogwe - Matha John Mkupasi
3. Nyang'wale- Hamim Buzohera Gwiyama
4. Geita - Herman C. Kipufi
5. Chato - Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
1. Mufindi - Jamhuri David William
2. Kilolo - Asia Juma Abdallah
3. Iringa - Richard Kasesela
KAGERA
1. Biharamulo- Saada Abraham Mallunde
2. Karagwe - Geofrey Muheluka Ayoub
3. Muleba - Richard Henry Ruyango
4. Kyerwa - Col. Shaban Ilangu Lissu
5. Bukoba - Deodatus Lucas Kinawilo
6. Ngara - Lt. Col. Michael M. Mtenjele
7. Missenyi - Lt. Col Denis F. Mwila
KATAVI
1. Mlele - Rachiel Stephano Kasanda
2. Mpanda - Lilian Charles Matinga
3. Tanganyika- Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA
1. Kigoma - Samsoni Renard Anga
2. Kasulu - Col. Martin Elia Mkisi
3. Kakonko - Col. Hosea Malonda Ndagala
4. Uvinza - Mwanamvua Hoza Mlindoko
5. Buhigwe - Col. Elisha Marco Gagisti
6. Kibondo - Luis Peter Bura
KILIMANJARO
1. Siha - Onesmo Buswelu
2. Moshi - Kippi Warioba
3. Mwanga - Aaron Yeseya Mmbago
4. Rombo - Fatma Hassan Toufiq
5. Hai - Gelasius Byakanwa
6. Same - Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI
1. Nachingwea- Rukia Akhibu Muwango
2. Ruangwa - Joseph Joseph Mkirikiti
3. Liwale - Sarah Vicent Chiwamba
4. Lindi - Shaibu Issa Ndemanga
5. Kilwa - Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA
1. Babati - Raymond H. Mushi
2. Mbulu - Chelestion Simba M. Mofungu
3. Hanang' - Sara Msafiri Ally
4. Kiteto - Tumaini Benson Magessa
5. Simanjiro - Zephania Adriano Chaula
MARA
1. Rorya - Simon K. Chacha
2. Serengeti - Emile Yotham Ntakamulenga
3. Bunda - Lydia Simeon Bupilipili
4. Butiama - Anarose Nyamubi
5. Tarime - Glodious Benard Luoga
6. Musoma - Dkt. Vicent Anney Naano
MBEYA
1. Chunya - Rehema Manase Madusa
2. Kyela - Claudia Undalusyege Kitta
3. Mbeya - William Ntinika Paul
4. Rungwe - Chalya Julius Nyangidu
5. Mbarali - Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO
1. Gairo - Siriel Shaid Mchembe
2. Kilombero - James Mugendi Ihunyo
3. Mvomero - Mohamed Mussa Utali
4. Morogoro - Regina Reginald Chonjo
5. Ulanga - Kassema Jacob Joseph
6. Kilosa - Adam Idd Mgoyi
7. Malinyi - Majula Mateko Kasika
MTWARA
1. Newala - Aziza Ally Mangosongo
2. Nanyumbu - Joakim Wangabo
3. Mtwara - Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
4. Masasi - Seleman Mzee Seleman
5. Tandahimba- Sebastian M. Walyuba
MWANZA
1. Ilemela - Dkt. Leonald Moses Massale
2. Kwimba - Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
3. Sengerema- Emmanuel Enock Kipole
4. Nyamagana- Mary Tesha Onesmo
5. Magu - Hadija Rashid Nyembo
6. Ukerewe - Estomihn Fransis Chang'ah
7. Misungwi - Juma Sweda
NJOMBE
1. Njombe - Ruth Blasio Msafiri
2. Ludewa - Andrea Axwesso Tsere
3. Wanging'ombe- Ally Mohamed Kassige
4. Makete - Veronica Kessy
PWANI
1. Bagamoyo - Alhaji Majid Hemed Mwanga
2. Mkuranga - Filberto H. Sanga
3. Rufiji - Juma Abdallah Njwayo
4. Mafia - Shaibu Ahamed Nunduma
5. Kibaha - Asumpter Nsunju Mshama
6. Kisarawe - Happyness Seneda William
7. Kibiti - Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA
1. Sumbawanga - Dkt. Khalfan Boniface Haule
2. Nkasi - Said Mohamed Mtanda
3. Kalambo - Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA
1. Namtumbo - Luckness Adrian Amlima
2. Mbinga - Cosmas Nyano Nshenye
3. Nyasa - Isabera Octava Chilumba
4. Tunduru - Juma Homela
5. Songea - Polet Kamando Mgema
SHINYANGA
1. Kishapu - Nyambonga Daudi Taraba
2. Kahama - Fadhili Nkulu
3. Shinyanga - Josephine Rabby Matiro
SIMIYU
1. Busega - Tano Seif Mwera
2. Maswa - Sefu Abdallah Shekalaghe
3. Bariadi - Festo Sheimu Kiswaga
4. Meatu - Joseph Elieza Chilongani
5. Itilima - Benson Salehe Kilangi
SINGIDA
1. Mkalama - Jackson Jonas Masako
2. Manyoni - Mwembe Idephonce Geofrey
3. Singida - Elias Choro John Tarimo
4. Ikungi - Fikiri Avias Said
5. Iramba - Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE
1. Songwe - Samwel Jeremiah
2. Ileje - Joseph Modest Mkude
3. Mbozi - Ally Masoud Maswanya
4. Momba - Juma Said Irando
TABORA
1. Nzega - Geofrey William Ngudula
2. Kaliua - Busalama Abel Yeji
3. Igunga - Mwaipopo John Gabriel
4. Sikonge - Peres Boniphace Magiri
5. Tabora - Queen Mwashinga Mlozi
6. Urambo - Angelina John Kwingwa
7. Uyui - Gabriel Simon Mnyele
TANGA
1. Tanga - Thobias Mwilapwa
2. Muheza - Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
3. Mkinga - Yona Lucas Maki
4. Pangani - Zainab Abdallah Issa
5. Handeni - Godwin Crydon Gondwe
6. Korogwe - Robert Gabriel
7. Kilindi - Sauda Salum Mtondoo
8. Lushoto - Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.

Na Mwandishi wetu

KLABU ya Simba imetoa taarifa kufuatia mjadala unaoendelea kuhusu malalamiko ya Yanga kuwa wekundu hao wanawafanyia mtima nyongo kumruhusu beki Hassan Kessy aruhusiwe kuitumikia Yanga.

Hii hapa ni taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari.


Awali ya yote klabu inaendelea kutoa pongezi kwa ndugu zetu waislaam wanaoendelea kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, tunaamini Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kwa ibada hiyo muhimu.

Ndugu wanahabari katika siku za karibuni hususan kuelekea mchezo wa Yanga na klabu kutoka DR Congo, TP Mazembe Englebert kumekuwa na maneno mengi kutoka klabu ya Yanga yakiishutumu klabu yetu kuhusiana na kutokutoa ruhusa kwa mchezaji Hassan Ramadhani 'Kessy' na pia kuhusiana na namna mashabiki watakavyokaa majukwaani siku ya mchezo huo Jumanne ya wiki hii.

Klabu ya Simba kwa makusudi kabisa inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na mambo hayo mawili yanayoleta sintofahamu miongoni mwa wadau wa mchezo huu murua wa kandanda.

Hakuna barua yoyote ambayo klabu ya Yanga imetuandikia kuhusiana na suala la mchezaji huyo pia hakuna hata mazungumzo yaliyofanyika baina ya viongozi wa klabu hizi ili kutuomba walau kwa mdomo kama taratibu zinavyotaka.
Ikumbukwe Simba huwa haina tatizo kuruhusu matakwa binafsi ya mchezaji na nyote mnajua utamaduni huo wa klabu yetu.

Kwa wasiofahamu mwaka 1998 klabu ya Simba iliwaazima Yanga  wachezaji watatu ili wacheze hatua ya makundi kama hii ya klabu bingwa Afrika, wachezaji hao ni Shaban Ramadhani, Monja Liseki na Alphonse Modest, sasa jiulize kama tuliweza kuwaazima wachezaji vipi tushindwe kumruhusu mchezaji waliyemsaini?

Pamoja na maneno yao ya kuudhi Simba ni waungwana wa kutosha na wao wasitumie ukimya wetu kuwapotosha wanachama na washabiki wao eti tumewakatalia kuwajibu barua ya kuhusu Kessy.
Msimamo wetu kuhusiana na jambo hili unategemea uungwana wao tu.

Pia Yanga kupitia msemaji wao wamenukuliwa kuwa kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe watakaa kwenye majukwaa yote hata yale ambayo kwa utamaduni wa uwanja wa taifa hukaliwa na mashabiki wa klabu yetu.

Tunafahamu kuwa kauli hii ina nia ya kuchochea vurugu kubwa kwenye mchezo huo na sote tunajua athari ya vurugu michezoni, tunawashauri Yanga wasijaribu kuleta mashabiki wao kwenye majukwaa wanayokaa washabiki wa Simba ili kuleta amani siku hyo ya mchezo. Matarajio yetu vyombo vinavyohusika vitasimamia kwa ukaribu jambo hilo.

Mwisho ingawa si kwa umuhimu klabu haimzuii yoyote kushangilia timu yoyote siku ya mchezo huo kama ilivyo desturi ya wao Yanga kushangilia klabu yoyote inayocheza na Simba hususan wageni toka nje kama ilivyokuwa miaka michache nyuma ambapo walishangilia na kuvaa jezi za TP Mazembe.

Waarabu wana msemo wao maarufu "KAMA TUDINI TUDANI" kama ulivyofanya na wewe utafanyiwa hivyo hivyo.