Tuesday, June 28, 2016

Sweeden imefungua Barabara ya Umeme(eHighway) kwa magari Makubwa!


Pengine Sweeden ndio inaweza ikawa nchi ya kwanza kuja na teknolojia hii kwa magari makubwa.Magari haya yanatembea katika barabara ambazo zimeunganishwa na nyaya za umeme. Kilicho fanyika ni kwamba magari hayo kwa juu yameunganishwa na nyaya ambazo zinaelea (zilizo shikiliwa na nguzo) Jina la barabara hiyo ni eHighway
   Magari ambayo yanapita katika barabara hiyo ni yale makubwa kabisa inasemekana wakati magarihayo yakiwa katika barabara hiyo yatakua hayatumii mafuta  lakini yakitoka nje ya barabara hiyo ya umeme ndiyo yatakuwa yanatumia mafuta kama kawaida

0 comments:

Post a Comment