Mbeya : Mkazi wa Tunduma, mkoani Songwe, Adam Kinyekile (34) ambaye alikuwa akitengeneza helikopta amepata mwaliko maalumu na wazungu kutoka Afrika Kusini kutembelea kiwanda chao cha kutengeneza chopa.
Kijana Kinyekile ambaye pia ni fundi magari alitumia ubunifu wake kuunda helikopta, kitu ambacho kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, George Mbijima akiwa mjini Tunduma alimtembelea kisha kuweka jiwe la msingi kwenye helikopta hiyo.
Hata hivyo baada ya taarifa za kijana huyo kurushwa kwenye vyombo vya habari , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilipiga marufuku kwa mtu yoyote kutojihusisha na utengenezaji au ubunifu wa ndege bila kufuata taratibu.
Onyo hilo lilionekana kumlenga Kinyekile kwa kazi yake aliyokuwa akiifanya jambo ambalo lilimfanya asiweze kuendelea na maboresho ya helikopta yake licha ya kudai ilikuwa imebaki kuruka.Akizungumza jana Adam Kinyekile alisema alhamisi ya wiki hii alitembelewa na wazungu walio dai ni Raia wa Afrika kusini kutoka katika kiwanda kinacho jishuhulisha na utengenezaji wa helkopta na walitaka kuonana naye ili wajionee kazi yake ambayo walidai waliiyona kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment