Tuesday, July 19, 2016

Wanachama Simba kujadili kumuuzia timu MO



Dar es Salaam. Mpango wa bilionea Mohamed Dewji (MO) kuinunua Simba umeanza baada ya uongozi wa klabu hiyo kuweka wazi kwamba suala hilo litajadiliwa katika mkutano mkuu utakaofanyika Julai 31.
Tayari Simba imeunda kamati kwa ajili ya kupokea maoni juu ya mpango huo, huku ikisisitiza kutomjadili MO pekee bali kampuni yoyote yenye fedha ambayo ina lengo la kununua hisa katika klabu hiyo.
Rais wa Simba, Evance Aveva aliliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba suala la MO limeanza kujadiliwa kwa kukusanya maoni ya wadau mbalimbali wa Simba juu ya azma ya bilionea huyo.
“Unajua MO si kama anahitaji kuidhamini Simba, la hasha, ingekuwa hivyo mbona tungekuwa tulishamalizana naye, anachokitaka MO ni kuinunua Simba, sasa kitu hiki hakipaswi kufanyiwa papara,” alisema Aveva na kuongeza.
“Tumeanza kwa kuiundia kamati ambayo inafanya kazi ya kutafuta maoni ya wana Simba juu ya mkakati huo, pia kwenye mkutano wetu mkuu tunatarajia kuwasilisha mpango huo na kujadiliwa na wanachama,” alisisitiza.
Bosi huyo wa Simba alifafanua kwamba katika mpango huo si kwa MO pekee, bali mchakato uliopo ni kutoa fursa kwa kampuni yoyote yenye fedha kununua hisa.
“Tunahitaji kuifanya Simba kuwa na mapato kuwa klabu tajiri, lakini kabla ya kuuza hisa lazima kwanza tushirikishane na wana Simba kutoa maoni yao ni nini kifanyike,” aliongez

0 comments:

Post a Comment