Thursday, August 4, 2016

JOTO LA MO SIMBA LATUA YANGA KIAINA.



Mabadiliko anayotaka mfanyabiashara Mohammed Dewji MO kwenye klabu ya Simba yanaonekana kuitia presha Yanga ambayo katika mkutano wa dharura wa Jumamosi, suala la mabadiliko huenda likawa ajenda.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameitisha mkutano huo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Jumamosi ambao kikatiba unaruhusiwa, baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wana mawazo ya kuibuka hoja ya mabadiliko ya kuifanya Yanga kampuni. Yanga ndiyo iliyoanza utaratibu huo mwaka 2007, ukaishia hewani kabla ya hivi karibuni MO akitaka amilikishwe asilimia 51 ya hisa za Simba. Katibu mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alipoulizwa kuhusu mkutano huo hakutaka kuzungumzia akidai haelewi ajenda itakuwa ipi na kuwataka wanachama wajitokeze kwa wingi kwani kila kitu kitajulikana huko. “Aaah wapi, mkutano wa Simba tumeusikia na kuona yale wanachama waliyoamua. Mkutano wetu (Yanga) utakuwa wa kawaida na zaidi tutautumia kuweka mikakati ya maendeleo kwa timu yetu. “Mkutano utakuwa na agenda za kawaida, tutajadili kuhusu uchaguzi wa viongozi uliofanyika miezi miwili iliyopita. Pia, wanachama watapata fursa ya kujadili maendeleo ya klabu ilikotoka, iliko na iendako,” alisema Baraka. Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali alisema hawajajua ajenda ni ipi, lakini suala la yanga kuwa kampuni huenda likachukua nafasi kubwa, Unajua sisi ndio tulianza mwaka 2007 lakini Madega tulimuita tukamueleza alikata na hata alivyo ingia Nchunga mchakato uliendelea ila haukufanikiwa na hata Manji alivyokuwa mfadhili alitaka mabadiliko naamini mkutano wa dharula ni suala litakalo jadiliwa, Alisema Akilimali.
 


0 comments:

Post a Comment