Bodi ya ligi ya
shirikisho la soka Tanzania Bara (TPBL) imemsimamisha kipa wa Azam, Razak
Abalora kuichezea timu hiyo kwa kosa la kumtolea lugha isiyofaa
mwamuzi Jonesia Rukyaa baada ya mechi dhidi ya Simba uliochezwa February 07
suala lake limepelekwa kamati ya nidhamu na maadili kujadiliwa.
Abalora inadaiwa Baada
ya Mpira kumalizika alimfuata Mwamuzi Rukya kumlalamikia kwa madai ya kuwanyima
Penati. Tayari azam Fc wamepokea barua ya kusimamishwa kwa Abalora kwa maana
hiyo Razak Abalora atakosa mchezo wa jioni ya leo dhidi ya Singida United katika
dimba la Azam Complex Chamazi Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment