Ilipo ishia...
Michezo ya utotoni ni moja ya mambo ambayo yalikua yakiimarisha tamaduni za kipare baadhi ya michezo ni kama Kajanja .Mchezo wa kujificha uliokuwa ukijulikana kama Kibe
Sehemu ya 4
Utamaduni
Kwa asili Wapare hupeleka vijana wa kiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia,
japo siku hizi utamaduni wa
kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache.
Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na
biashara,
ndiYo maana hata leo wana uchumi
mzuri katika viwango vya Tanzania.
Tamaduni, mila na desturi za wapare zimekuwa
zikifanana sana kwa koo karibu zote. Hapo kale Wapare pia waliweza kutengeneza
au kuifunga mvua
kwa shughuli za jadi, jambo ambalo wapo baadhi ya Wapare ambao mpaka leo
wanaweza. Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo, ambaye aliacha
uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupiga marufuku utawala wa jadi. Kiongozi huyo aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa
kuleta mvua.
Pia walikuwepo hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya
Same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata
mdudu
wala ndege
atakayeweza kutua eneo hilo. Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea
kama si kwisha kabisa.
Wapare pia wamekuwa wakihusishwa na imani za uchawi na
ushirikina
kama ilivyo kwa makabila mengine Tanzania, lakini suala hili ni la mtu binafsi
zaidi na si la jamii fulani peke yake kwa sababu ni imani ambazo zipo kote
Tanzania na hatuwezi kunyooshea kidole eneo fulani.
Kwa wapare walio wengi, uchawi na wizi vilipigwa
marufuku hadi kwenye matambiko. Mchawi na mwizi waliombewa wafe kama ikitokea
wapo kwenye jamii. Kuna utamaduni unaoitwa "mma" ambapo matambiko
yalifanyika mahali fulani na mwizi akaitwa pale yanapofanyikia kisha mwombaji
akaulizwa angependa mwizi apewe adhabu gani.
Kwa kawaida adhabu mbili kuu ndizo zilikuwepo:
kumfanya mwizi augue sana kwa muda mrefu kabla ya au kumuuwa mara moja.
Mwombaji akimamua mwizi auawe basi kwa vile anaonekana kwenye matambiko,
mtaalamu wa matambiko humuuwana akafariki mida hiyohiyo huko aliko. Tatizo la
kuu la "mma" ni kwamba lilikuwa linaua watu wote wa ukoo wa mwizi au
mchawi (lakini mwizi akiwa wa kwanza). Ni mpaka watakaopjua kuwa ni
"mma" ndipo watafanya matambiko ya kutoa mnyama kafara kwa ajili ya
kuzima athari za mma. Kwenye kuuzima mma ni lazima aliyedhulumiwa ahusishwe
kwenye matambiko ikiwa ni pamoja na kuombwa radhi, vinginevyo mma hautazimika.
Athari zingine za "mma" ni kwamba aliyeomba tambiko hilo (yaani
aliyeibiwa au aliyedhulumiwa), ni lazima atoe kafara mnyama kama vile kondoo au
ng'ombe kabla na baada ya tambiko. Baada ya mwizi kufa ni lazima mwombaji atoe
mnyma kafara ili kuzima madhara ya "mma". Vinginevyo vifo vitokanavyo
na mma humrudia mwombaji na ukoo wake.
Kuna watu maalum waliokuwa wamebobea kwenye mambo ya
"mma". Kwa sababu ya matambiko hayo ndio maana wapare wengi si wezi -
japokuwa siku hzi baadhi yao wamejiingiza kwenye wizi. Tambiko lingine
linalofanana na hilo liliitwa " kubigha nyungu" (kwa Kiswahili -
kupiga chungu). Chungu hicho kilipigwa kama tambiko la kumuuwa mtu aliyedhulumu
(au ukoo wao uliohusika na dhuluma) watu wengine. Chungu hicho hupigwa chini
mara moja kwa kishindo, ambapo tendo hilo lilambatana na matambiko fulani. Mara
chngu hicho kipasukapo kwa mshidno ndipo ukoo wa waliodhulumu huanza kufa
mmojammoja. Iliaminika kwamba kitendo cha chungu kusambaratika vipande vipande
ndivyo na ukoo uliodhulumu husambaratika. Tambiko hili lilichangia kwa kiasi
kikubwa Wapare kuwa kabila la wapenda haki. Nasikia tambiko hili lilikuwepo
hata kwa makabila ya jirani kama vile wasambaa, Wameru n.k. Hata hivyo
matambiko hayo kwa sasa hivi hayapo. Yamebaki historia kwenye kabila la wapare
na hayo makabila mengine.
Ngoma za jadi zilipigwa kwa
matukio maalumu kama kwenye jando au unyago, pia nyimbo za Kipare zilitumika
katika ngasu kama harusi na
sherehe
nyingine na kupendezesha tukio husika. Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata
kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.
Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali, hadithi,
maigizo n.k. wakati wa mapumziko na matukio fulani. Hali hii
imepelekea kuwepo wasanii wengi maarufu wa maigizo na nyimbo kama Halima
Madiwa, Jacob Steven (JB), Sinta, Sara Mvungi, Roma Mkatoliki na wengineo wengi
Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi Wapare walikuwa
wakiamini tiba za mitishamba
kwa kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu, kirutu n.k. Ipo miti maarufu kama
mwori ambayo ilitumika. Mchango wa dawa za mitishamba kwa watoto na watu wazima
ulionesha mafanikio tangu zamani na hata sasa.
Samaki
pia ni kipenzi cha Wapare wengi na ndiyo maana utawasikia watani wao wakuu
yaani Wachaga wakiwatania kuwa Wapare wanakula ugali kwa picha ya samaki. Huu ni utani ulioasisiwa na wachagga baada
ya kutembelea kaya nyingi za wapare na kukuta wamehifadhi samaki. Hapo ndipo
mchagga mmoja alisikika akisema "Yesu yaani wapare wanapenda samaki, kila
nyumba unayoingia utakutana na samaki. Yaani siku wakikosa samamki watakula
ugali kwa picha ya samaki". Utani huo ulikuzwa na wachagga hadi ukaonekana
kama ni kweli, ukizingatia wachagga wametapakaa nchi nzima.
Hata hivyo wapare nao wana utani wao kwa wachagga
unaosema "Muagha wedi ni ula efwie". Yaani "mchagga mzuri ni
yule aliyekufa" wakimaanisha kwamba wachagga wote ni walaghai na
wadhulumishi wakati wote wa maisha yao. Ni mpaka atakapokufa ndipo ulaghai na
udhulumishi wake vitaisha.
Mito ya Upare
Kuna mto
Yongoma,Mto shengena, Hingilili, Mhoke vuta, Nakombo, Rika, Mweta nano hii mito
yote iko Pare ya kusini. Katika mto Hingilili kuna maporomoko makubwa na
yanayosadikiwa kuwa marefu kuliko yale ya Victoria Falls, haya yanajulikana kama Ndurumo
yapo eneo la Gonja Bombo umbali mfupi kutoka mtaa wa Mang'ang'a katika eneo
linaloitwa Mbula.
Maziwa na mabwawa
Kuna ziwa
Jipe, bwawa la Nyumba ya Mungu Bwawa la dibwi na Kalemawe n.k.
Maeneo mazuri ya kutembelea
- Mbuga ya Mkomazi
- Bwawa la Nyumba ya Mungu
- Msitu wa asili wa Shengena
- Bwawa la Kalimawe
- Maporomoko ya Ndurumo - Gonja
Bombo
- Msitu wa Ngagheni Mpinji- Vudee
uliokuwa wa matambiko karne ya 17 mpaka 19
- Mlima wa Masheko Ndolwa-Vudee
uliokuwa na Matambiko ya Wapare
- Jabali la Mhewe -Vudee
lililopasuliwa na wananchi wa Vudee kuwezesha barabara kupita miaka ya
1960 na 1961.
- Msitu wa Wambugu ulioko karibu
na Dangaseta- Mwembe uliotumika kwa matambiko ya kabila linaloishi Lushoto
Tanga-hadi leo wachache wao bado hufika kutambika pale.
- Msitu na chanzo cha maji ya
kwachegho sehemu ambayo ni ya ajabu maana ndio sehem pekee ambayo maji
yanaonekana kutiririka kuelekea sehemu ya muinuko
- Mlima Kindoroko
Usikose kusoma makala mbalimbali juu ya maajabu mbalimbali yanayo patikana ndani ya Tanzania baada ya makala hii kwisha