Taarifa
kutoka katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini Zambia
ukiwemo lusakatimes.com leo November 7 2016 imeripoti taarifa
kuhusiana na aliyekuwa kocha mkuu wa Zesco United George Lwandamina kujiuzulu
nafasi hiyo ambapo mkataba wake ungemalizika January 2017, kitendo hicho
kinadaiwa ni dalilia za kujiunga na Yanga.
Zaidi
ya mwezi Lwandamina amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga kuchukua nafasi ya muholanzi Hans
van Pluijm, maamuzi ya Lwandamina kuachia
nafasi hiyo yamebarikiwa na uongozi wa Zesco na yamethibitishwa na CEO wa Zesco Justin Mumba na afisa habari wao Katebe Chengo na kusema nafasi yake itarithiwa na
msaidizi wake Tenant Chembo hadi mwisho wa msimu
Lwandamina alikuwepo Dar es Salaam October 24 akidaiwa kufanya
mazungumzo na viongozi wa Yanga licha ya yeye kukanusha na kusema
alikuja kwa biashara zake binafsi, Lwandamina alijiunga na Zesco United 2014 na ameipa mataji mawili ya
Ligi Kuu, Barclay Cup, Charity Shield na ameiongoza timu hiyo 2016
kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika zipo taarifa
ambazo sio rasmi kuwa siku ya juma mosi huenda benchi la ufundi la yanga
likavunja rasmi
0 comments:
Post a Comment