Tuesday, January 31, 2017

Matokeo kidato cha nne 2016/2017






MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016



BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 31, 2017 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Sekondari, Kidato cha Nne kwa mwaka 2016, mtihani ambao ulifanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.44 ukilinganishwa na ule wa mwaka jana.

Katika matokeo hayo, shule za Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam zimeonekana kung’ara zaidi kwa kushika nafasi za juu wakati huohuo shule 6 za Dar es Salaam zikishika nafasi 10 za mwisho katika matokeo hayo.

SHULE ZILIZOINGIA 10 BORA KITAIFA:
Feza Boys Sec School – Dar es Salaam
St. Francis Girls Sec School -Mbeya
Kaizirege Junior Sec School – Kagera
Marian Gilrs Sec School – Pwani
Marian Boys Sec School- Pwani
St. Aloysius Girls Sec School – Pwani
Shamsiye Boys Sec School – Dar es Salaam
Anuarite Girls Sec School- Kilimanjaro
Kifungilo Girls Sec School- Tanga
Thomas More Machrina Sec School – Dar es Salaam

SHULE ZA DAR ES SALAAM ZILIZOSHIKA NAFASI 10 ZA MWISHO:-

Kitonga Sec School

Nyeburu Sec School

Mbopo Sec School

Mbondole Sec School

Somangila Day Sec School

Kidete Sec School
Ingia hapo chini kwa matokeo zaidi
http://necta.go.tz/

Friday, January 27, 2017

Baadhi ya watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuchunguzwa kwa ubadhilifu wa mamilion ya Fedha


Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka kuwachukulia hatua watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa waliohusika na upotevu wa fedha za maendeleo ambapo zaidi ya shilingi milioni 700 zilipelekwa katika halmashauri hiyo kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo shilingi milioni 300 za ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri hiyo.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri alipokuwa katika ziara yake ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.
Pamoja na agizo hilo Waziri Mkuu Majaliwa pia ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) kuhakikisha inashirikiana katika kufanya uchunguzi ili kubaini watu waliohusika na upotevu huo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametahadharisha kuwa Serikali haitowavumilia watumishi wote wanaojihusisha na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma. Amewataka watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na maadili pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia vizuri fedha za maendeleo zinazopelekwa kwenye maeneo yao na kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Awali akiwa njiani kuelekea Ludewa Mjini akitokea katika kata ya Mundindi Waziri Mkuu alisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali ambao waliiomba Serikali iwasaidie kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji.

Odinga adai njama ya wizi wa kura uchaguzi mkuu Kenya


 
Miezi saba kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya, kiongozi wa upinzani Raila Odinga ameituhumu serikali ya Jubilee kwa kuendeleza ufisadi wa hali ya juu na kupanga njama ya kuiba kura kwenye uchaguzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Ijumaa, Raila Odinga, kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani NASA, alidai kuwa serikali ya Uhuru Kenyatta inapora mali ya umma wakati ambapo anahisi kwamba huenda ikashindwa kwenye uchaguzi ujao.

"Nilipozungumzia kashifa ya "NYS" walisema nawaonea wivu juu ya maendeleo wanayofanya, nilipozingumzia kashifa ya "Eurobond" wakatishia kuniweka kizuizini na hatimaye hata mkaguzi mkuu wa mahesabu anasema hajaona fedha hizo kwenye vitabu vya mahesabu katika Benki Kuu,” alisema  Odinga.

Kuhusu zoezi la kusajili wapiga kura ambalo ni la mwisho kabla uchaguzi mkuu kufanyika, kiongozi huyo wa upinzani alidai kuwa serikali inatumia maafisa wa utawala kuhimiza usajili katika ngome za jubilee. Raila alisema maafisa hao hao katika ngome za upinzani wanatishwa dhidi ya kufanya hivyo.

Viongozi wa chama tawala cha Jubilee hata hivyo wameyapuuza madai ya Raila. "Ati anasema kuzunguka kwangu kuomba watu wajiandikishe, ni kuiba kura. Hiyo siasa ya vitisho tuache, watu wakitaka tushindane, tushindane kwa sera na yeye awaambie watu ni atawafanyia," alisema Rais Kenyatta katika mmoja ya mikutano yake.

Hayo yanaendelea huku zoezi la kusajili wapiga kura ambayo ni awamu ya mwishi likiingia wiki ya pili sasa. Kila upande unafanya kampeni ya kushawishi wapiga wananchi katika ngome zao kujisajili kama wapiga kura huku Tume ya Uchaguzi IEBC ikisema haitaongeza muda wa usajili.

"Hatuoni tukiongeza muda huu kwa hivyo ikiwa hutajisalili wakati huu hutaweza kushiriki kwenye uchaguzi,” alisema mkurugenzi wa IEBC Ezra Chiloba.

Tume ya uchaguzi inalenga kusajili wapigakura wapya wapatao milioni 6 ingawaje kufikia sasa ni takriban wapiga kura milioni moja pekee waliosajiliwa.

Uchaguzi mkuu ujao unaelekea kuwa kati ya mafahari wawili, Rais Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilee anayetetea kiti chake na mgombea wa muungano mpya wa upinzani wa National Super Alliance, NASA ambao mgombea wake bado hajatangazwa. Zaidi ya vyama 15 vya upinzani vimeungana na muungano wa CORD kubuni muungano mpya wa NASA.
 
chanzo DW HABARI

Thursday, January 26, 2017

Wimbo mpya wa John makini mp4


Sikiliza wimbo mpya wa John makini

Wednesday, January 25, 2017

Samatta aendelea kung`ra nchini Ubelgiji




Mbwana Samatta ameendelea kufanya kweli kwenye ligi ya Ubelgiji baada ya kuifungia tena timu yake ya KRC Genk wakati ilipo kuwa ikimenyana na Kortrijk huku Genk ikichomoka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Kortrijk kwenye mchezo wa ligi.ya Ubelgiji baada ya kuifungia tena timu yake ya KRC GENK, Timu hiyo ilio chomoka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Kortrijk kwenye mchezo wa ligi kuu nchini hapo

Ni goli la pili mfululizo baada ya siku chache zilizopita Samatta kuifungia timu yake bao pekee lililoipa pointi tatu za ugenini wakati ikicheza dhidi ya AS Eupen.

Samatta alifunga goli lake dakika ya 42 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Schrijvers na kuandika bao la pili.

Magoli mengine ya Genk yamefungwa na Siebe Schrijvers dakika ya 38 na Alejandro Pozuelo dakika ya 68 na kuipa Genk ushindi wa magoli 3-0. Katika ligi ya ubelgiji KRC Genk ipo nafasi ya nanne  kat ya timu kumi na sita ikiwa imejikusanyia point 34 kibindoni baada ya kushuka dimbani mara 22 na kushinda michezo 10 huku ikitoka sare michezo nanne na kupoteza michezo nanne