Thursday, June 29, 2017

Taifa Stars yafuzu hatua ya Robo fainali

Timu yaTaifa Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuingia hatua ya Robo fainali ya kombe la Halmashauri ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa miguu kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya Kulazimisha kwenda Sare ya 1-1 dhidi ya Mauritius kwa goli lililofungwa na Simon msuva dakika ya 68' dakika moja tu baada ya Mauritius kuandika goli la kuongoza (dk 67') kupitia kwa Kelvin Perticots, huku Angola nayo ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Malawi. 

Kwa matokeo hayo Tanzania inaongoza kundi 'A' kwa tofauti ya goli moja dhidi ya Angola ambayo nayo ina alama sawa na Tanzania kwa matokeo haya.Tanzania itakutana na Afrika Kusini katika Mchezo wa Robo Fainali tarehe 5 July.
Mungu ibariki Tanzania 

Saturday, June 24, 2017

Polisi Mara yawaasa wakazi wa Mkoa wa Mara kusherekea sikuku ya eid – el – fitr kwa amani,

   Jeshi la polisi mkoa wa Mara limejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu na kuwataka wananchi kusheherekea sikuku hii kwa amani, Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi wa polisi Jafari m. Ibrahim amesema vitendo vya kihalifu havina nafasi mkoani Mara na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha Sikukuu ya EID – EL – FITR ili kulinda maisha ya watu na mali zao dhidi ya wahalifu wanaotumia fursa hiyo kufanya vitendo viovu.
            Pia amewaasa Wananchi kutowaacha watoto wao kutembea peke yao wakati wa sikuu hii bila ya kuwa na waangalizi ili kuepusha majanga yoyote yanayoweza kutokea ikiwa ni pamoja na ajali zisizo za lazima.Hata hivyo Jeshi la polisi limejipanga kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yatakayo kuwa na mkusanyiko ya watu na kufanya doria za Miguu, Magari na pikipiki katika maeneo yote ya Mkoa wa Mara
          Aidha kamanda wa polisi Mkoa wa Mara ametoa onyo kali kwa mtu/kikundi chochote cha watu Kitakacho fanya au kusababisha  vurugu,fujo ama vitisho vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati wa  sherehe hizi, Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao

Friday, June 23, 2017

Mashabiki wa Yanga jiandaeni kuchoma jezi nyingine-Haji manara

        Msemaji wa klabu ya Simba Hajji Manara aliye fungiwa amewashangaa baadhi ya mashabiki wa Yanga kwa kitendo cha kuchoma moto jezi  aliyokua akiitumia Haruna Niyonzia ambaye kwasasa ameachana na klabu hiyo. Manara amesema kua kwa sasa bado na wajiandae kuchoma jezi nyingine zaidi kwani sio Niyozima pekeyake wapo baadhi ya wachezaji wengine watakao ungana na Niyozima. Hata hivyo manara hajafafanua ni wachezaji gani ambao wataungana na Haruna Niyozima .Hivi karibuni baadhi ya mashabiki wa yanga wamekua wakichoma moto jezi aliyokua akiitumia Haruna Niyonzima pindi alipokua akiitumikia klabu ya yanga kwakile walichodai ni kutokukubaliana na uwamuzi wa mchezaji huyo wa kuachana na klabu hiyo na kwenda upande wa pili.

         Manara amebainisha hayo kupitia katika ukurasa wake wa twitter sikumoja baada ya mashabiki hao kuiyandama jezi namba nane ya klabu yao ya yanga aliyokua akiitumia Haruna niyozima kwa kuichoma moto katika ukurasa wake manara ameandika maneno haya

       “Katika miaka ya karibuni wachezaji kadhaa wa simba walihamia Gongowazi hazikuchomwa moto jezi zao,Wenzetu ustarabu ziro ila wajiandae kuchoma nyingine `soon` kama mlivyo fanya mtafanyiwa the same”

Huu ni Ushabiki au Ugomvi?

         Baadhi ya mashabiki wa yanga wameonyesha kutokomaa kisoka, Hii ni baada ya kuonyesha  kitendo ambasho hakiendani na maswaala ya michozo. Mshabiki hao wamekua wakichoma moto jezi namba nane aliyokua akiitumia mchezaji Haruna niyozima wakati akiwa mchezaji wa yanga kwani kwasasa zipo tetesi amejiunga na watani wao wa jadi Simba sc. Swala la mchezaji kuhama timu huwa ni suala la kawaida duniani kote na ndio ajira ya mchezaji kwani huangalia nisehemu gani penye maslahi zaidi kifedha na kutimiza ndoto zake za badae.Kwaupande wa baadhi ya mashabiki wa yanga kwao naona imekua tofauti kwani tangu taarifa za kuondoka kwa Haruna Niyozima wazipate kumekua na baadhi ya matukio ya kuchoma moto jezi aliyokua akiivaa mchezaji huyo jezi namba nane kitendo kinachoonyesha kuwa mashabiki hao bado si wakomavu katika masuala ya ushabiki wa soka na ukizingatia mchezaji huyo hakuanzia kucheza mpira katika klabu ya yanga kwani hata wao walimsaliji toka timu nyingine na wala huko alikotoka mashabiki hawajafanya vitendo kama vyao.

       Aidha yapo mabo inabidi baadhi ya mashabi hao waige kutoka kwa watani wao Simba sc kwani kama ni kuchoma jezi za wachezaji ambao wamehama timu hiyo na kujiunga na Yanga Simba ndio wahanga wakuu kwa takwimu za haraka haraka wapo wachezaji kama Athumani idd,Hassani kessy Ibrahimu ajibu waliondoka Simba huku mashabiki watimu hiyo bado walikuwa na mapenzi na wachezaji hao ila hakuna hata mmoja aliye subutu kuchoma jezi ya wachezaji hao na badala yake jezi za wachezaji hao zimekua kama kumbukumbu kwa mashabiki wa sasa na hata wajao katika klabu hiyo.

Thursday, June 22, 2017

Kivuli cha Haruna Niyonzima chawatesa baadhi ya mashabiki wa yanga

Huenda inaweza kuchukua muda mrefu kwa baadhi ya mashabiki wa yanga kumsahau mjezaji wao kipenzi kwani Kuondoka kwa Haruna Niyonzima, kunaonekana kumewaumiza na kuwakera sana baadhi ya mashabiki wa Yanga mpaka kufikia kuchoma jezi yake. Niyonzima anaelekea Msimbazi. mbaya zaidi ni kwamba mashabiki hao nikama wanatembea na kivuli cha mchezaji huyo kwani kila waiyonapo jezi namba nane ya timu yao huwakumbusha mbali na wengine kuamua kuichoma moto jezi hiyo.

Yaondoka na matumainiTaifa Stars

Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kinaondoka leo Alhamisi Juni 22, 2017 kwenda nchini Afrika Kusini katika michuano ya kuwania Kombe la Castle Cosafa.Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, ilikuwa kambini Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam, tangu Jumapili Juni 18, mwaka huu.Taifa Stars imeandaliwa kwa michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika. Tanzania si mwanachama wa Cosafa, lakini imealikwa katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu.
          Taifa Stars imepangwa kundi A na timu za Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, kikosi kinachoondoka leo ni makipa Aishi Salum Manula  (Azam FC), Benno David Kakolanya  (Young Africans SC) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Salum Kapombe    (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young Africans SC) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans FC).
        Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.Kadhalika wako viungo wa kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).Katika safu ya ushambuliaji wamo Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).

Taifa Stars yaondoka na Matumaini