Friday, June 23, 2017

Huu ni Ushabiki au Ugomvi?









         Baadhi ya mashabiki wa yanga wameonyesha kutokomaa kisoka, Hii ni baada ya kuonyesha  kitendo ambasho hakiendani na maswaala ya michozo. Mshabiki hao wamekua wakichoma moto jezi namba nane aliyokua akiitumia mchezaji Haruna niyozima wakati akiwa mchezaji wa yanga kwani kwasasa zipo tetesi amejiunga na watani wao wa jadi Simba sc. Swala la mchezaji kuhama timu huwa ni suala la kawaida duniani kote na ndio ajira ya mchezaji kwani huangalia nisehemu gani penye maslahi zaidi kifedha na kutimiza ndoto zake za badae.Kwaupande wa baadhi ya mashabiki wa yanga kwao naona imekua tofauti kwani tangu taarifa za kuondoka kwa Haruna Niyozima wazipate kumekua na baadhi ya matukio ya kuchoma moto jezi aliyokua akiivaa mchezaji huyo jezi namba nane kitendo kinachoonyesha kuwa mashabiki hao bado si wakomavu katika masuala ya ushabiki wa soka na ukizingatia mchezaji huyo hakuanzia kucheza mpira katika klabu ya yanga kwani hata wao walimsaliji toka timu nyingine na wala huko alikotoka mashabiki hawajafanya vitendo kama vyao.

      

       Aidha yapo mabo inabidi baadhi ya mashabi hao waige kutoka kwa watani wao Simba sc kwani kama ni kuchoma jezi za wachezaji ambao wamehama timu hiyo na kujiunga na Yanga Simba ndio wahanga wakuu kwa takwimu za haraka haraka wapo wachezaji kama Athumani idd,Hassani kessy Ibrahimu ajibu waliondoka Simba huku mashabiki watimu hiyo bado walikuwa na mapenzi na wachezaji hao ila hakuna hata mmoja aliye subutu kuchoma jezi ya wachezaji hao na badala yake jezi za wachezaji hao zimekua kama kumbukumbu kwa mashabiki wa sasa na hata wajao katika klabu hiyo.



        


0 comments:

Post a Comment