Jeshi la polisi mkoa wa Mara limejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu na kuwataka wananchi kusheherekea sikuku hii kwa amani, Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi wa polisi Jafari m. Ibrahim amesema vitendo vya kihalifu havina nafasi mkoani Mara na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha Sikukuu ya EID – EL – FITR ili kulinda maisha ya watu na mali zao dhidi ya wahalifu wanaotumia fursa hiyo kufanya vitendo viovu.
Pia amewaasa Wananchi kutowaacha watoto wao
kutembea peke yao wakati wa sikuu hii bila ya kuwa na waangalizi ili kuepusha majanga yoyote yanayoweza
kutokea ikiwa ni pamoja na ajali zisizo za lazima.Hata hivyo Jeshi la polisi
limejipanga kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yatakayo kuwa na mkusanyiko ya
watu na kufanya doria za Miguu, Magari na pikipiki katika maeneo yote ya Mkoa
wa Mara
Aidha kamanda wa polisi Mkoa wa Mara
ametoa onyo kali kwa mtu/kikundi chochote cha watu Kitakacho fanya au
kusababisha vurugu,fujo ama vitisho
vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati wa sherehe hizi, Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
0 comments:
Post a Comment