Msemaji wa timu ta Simba Haji Manara na mchambuzi wa michezo wa redio clous Shaffih Dauda wameingia katika vita ya kimichezo, Choko choko ilianzia pale
Simba SC ilipofungwa, ambapo Shaffih alianza kuposti picha kwenye ukurasa wake
wa Instagram akihoji kuhusu mwenendo wa klabu hiyo tangu ulipoanza mwaka 2018.
Shaffih alianza kuposti picha
mbalimbali za Simba SC na kuuliza kama kuna uwezekano wa klabu hiyo kukwea
ndege msimu ujao akiimanisha kufuzu kushiriki michuano ya kimataifa huku
akihimiza mabadiliko ndani ya timu hiyo kuwa yaanzie kwa Haji Manara kwani ndiye
anayewapotosha mashabiki wa Simba SC.
Uvumilivu ukamshinda Haji
Manara ndipo alipoamua kumtolea uvivu Shaffih Dauda kwa kumwambia kuwa chuki
zake binafsi na klabu ya Simba asiwaambukize mashabiki wengine kwa kuposti vitu
vya kichochezi na kumuonya kuwa endapo ataendelea basi atamuadabisha yeye
pamoja na Radio Clouds FM.
“Tunajua wewe una ugomvi wako binafsi na baadhi
ya viongozi wa Simba. Lakini usitafute ugomvi na wanasimba wote, Sie kufungwa
sio wa kwanza na hatutakuwa wa mwisho. Unatumia muda mrefu kuittack Simba na
post zako za kijinga. Tunajua unajikomba kwa Yanga baada ya kutaka
kukupiga kwenye issue ya Akilimali, jipime bro vinginevyo utavunja heshma yako
na ya clouds media pia.”ameandika Haji Manara.
Shaffih Dauda naye akaona sio
vyema kukaa kimya akaamua kumjibu kwa kumwambia Manara asimtumie yeye kama
kichaka cha kujificha, Kwani Simba ilipofungwa na Green Worriors Manara
alitumia kichaka cha Omog kuficha makucha.
“Kaka usinitumie mimi kichaka cha wewe
kujifichia, last time Simba imefungwa na Green Worriors uljifichia
kwa Omoga katimuliwa sasa hivi hauna mahala pa kujifichia.“ameandika
Shaffih Dauda na kumtaka Haji Manara ajiuzulu nafasi yake
“Ilibidi wakati huu unaozungumza uwe umeachia
nafasi yako kwasababu umekuwa ukiwadanganya kwa kuwapa matumaini hewa wana
Simba.“amemaliza Shaffih Dauda.
Hata hivyo mashabiki wengi wa
Simba SC wamemshambulia Shaffih Dauda kwa kumuita mchochezi na wengine
wakimtaka kutomshambulia Manara amuache afanye kazi yake huku baadhi ya watu
wakimshauri Shaffih aendelee kufanya kazi yake ya uchambuzi aachane na uongozi
wa Simba.