Kuibuka kwa ufa mkubwa katika eneo la
Suswa katika Bonde la Ufa kusini magharibi mwa Kenya kumezua wasiwasi kuhusu
uthabiti wa eneo la Afrika Mashariki kijiolojia.Wataalamu wanasema kutokea kwa
ufa huo katika jimbo la Nakuru ni shughuli ya kijiolojia inayochukua muda mrefu
ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda.Hilo limezua hatari ya kuanza kutokea tena
kwa mitetemeko ya ardhi na milipuko ya vilkano.Wanajiolojia wanasema baada ya
mamilioni ya miaka, bara la Afrika litapasuka na kuwa vipande viwiliSehemu ya
mpasuko itakuwa kwenye Bonde la Ufa jambo ambalo linazua uwezekano wa Kenya na
Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika,
kujitenga na bara la Afrika.Mwanajiolojia David Adede ameambia BBC kwamba ufa
huo ni sehemu ya kutengana kwa vipande viwili vikubwa vya bara Afrika ambako
kutasababisha bara Afrika kutengana na kuwa mabara mawili.Amesema shughuli hiyo
imekuwa ikiendelea kwa muda lakini dalili zake zilikuwa zinafichwa na majivu ya
volkano ambayo polepole yamekuwa yakiziba ufa kila unapotokea.
"Maji ya mvua yamesomba majivu hayo
pamoja na mchanga na kuufanya ufa huo kuonekana zaidi," amesema.
Anasema vipande hivyo vimekuwa vikitengana
"katika kasi ya sentimita mbili kila mwaka."Kipande kilicho na sehemu
kubwa ya bara hufahamika kama Kipande cha Nubia na kipande cha pili hufahamika
kama Kipande cha Somalia.Dkt James Hammond kutoka kwa Idara ya Sayansi na
Uhandisi wa Dunia kutoka chuo cha Imperial College London alinukuliwa na jarida
la mtandaoni la Mail & Guardian akisema: "Katika miaka milioni kadha
ijayo, shughuli hii itakamilika na kuigawa Afrika mara mbili, na kuunda bahari
mpya hapo katikati na bara jingine. Ukitumia jiografia ya sasa, bara hilo jipya
litashirikisha Somalia, nusu ya Ethiopia, Kenya na Tanzania."Baadhi ya
wanajiolojia wanakadiria kwamba huenda mpasuko huu ukayabeba pia mataifa ya
Uganda, Rwanda, Burundi na maeneo ya Malawi na Msumbiji.Mwanajilojia Dereje
Ayalew kutoka Chuo Kikuu cha Addis Ababa Ethiopia aliambia jarida hilo kwamba
dalili za kutokea kwa bahari zimeanza kuonekana katika maeneo ya jangwani ya
Ethiopia, eneo la Afar ambalo pia linahusisha baadhi ya maeneo ya Eritrea na
Djibouti.
Mwaka 2005, alisema
tayari nyufa nyingi zimeanza kutokea na ardhi imebonyea kwa hadi mira 100
Ufa huo ulianza kuonekana wiki moja
iliyopita baada ya mvua kubwa kunyesha na barabara ya Mai Mahiu kwenda Narok
ikakatika eneo lenye ufa huo.Awali, wengi waliamini ufa huo uliotokea Jumanne
wiki iliyopita eneo la Karima ambalo linapatikana kilomita sita kutoka mji wa
Mai Mahiu ulitokana na mvua kubwa.
Ufa huo uliokuwa umeikata barabara hiyo
ulikuwa umeenea umbali wa mita 700.
Maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Barabara
Kenya (KeNHA) wakishirikiana na mkandarasi kutoka China anayejenga reli ya
kisasa, walifika eneo hilo na kuziba ufa.
Baada ya uchunguzi, ilibainika kwamba
ulitokana na shughuli ya kijiolojia chini ya ardhi ambayo ilihusisha mvutano wa
vipande vikubwa vya ardhi.Siku chache baadaye Jumapili, ufa huo uliendelea
kupanuka na kuathiri barabara hiyo tena jambo lililosababisha magari yenye
kubeba mizigo mizito kutoweza kupita.
Aidha, ufa huo ulianza kuathiri nyumba
za wakazi."Mkandarasi na kundi la wahandisi wamewekwa hapo kwa sasa na
watasalia kuendelea kufuatilia yanayojiri kutokana na shughuli za kivolkano
ambazo zilisababisha ufa huo," alisema naibu mkurugenzi wa mawasiliano wa
KeNHA Charles Njogu baada ya ukarabati huo mara ya kwanza.Bw Adede amesema
hatua ya kuziba ufa huo kwa sasa itasaidia kwa muda mfupi tu.Ufa huo umepitia
katika baadhi ya nyumba na mashamba ya watu
Mmoja wa walioathirika
ni Eliud Njoroge,77, ambaye ameambia anadai kuishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka
20.Anasema amelazimika kuibomoa nyumba yake na sasa analazimika kuishi kama
'mkimbizi' kwa jirani yake.Baadhi ya waandishi waliofika katika baadhi ya
maeneo ya ufa huo wamedai ufahuo unaupana wa mita 20 na kina cha hadi futi 50.
Wataalamu wametahadharisha kwamba nyufa zaidi zinaweza kuendelea
kuonekana katika baadhi ya maeneo ya Bonde la Ufa.
chanzo BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment