Wednesday, October 26, 2016

Baraza la Michezo nchini (BMT) lasitisha mabadiliko Simba na Yanga



          Baraza la Michezo nchini (BMT) limeagiza vilabu vyote vinavyoendelea na mchakato wa kubadilisha umiliki wa timu kutoka kwa wanachama kwenda kwenye umiliki wa hisa na ukodishwaji kusitisha hadi hapo marekebisho ya katiba zao yatakapofanyika.Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema, wahusika wanatakiwa kufuata sheria zilizopo katika mabadiliko wanayotaka kuyafanya na pia mchakato huo unaendelea kutengeneza makundi ya wapenzi na wanachama ambao wanajikita katika mijadala na kuzidi kuibomoa jamii badala ya kuijenga na kuimarisha michezo nchini.

        Kiganja amesema, wanapenda kuona wahusika wanafuata sheria na taratibu za nchi katika kufikia malengo yao na kuendelea na mchakato huo kabla ya taratibu za kurekebisha katiba zao kisheria ni kosa na hatua stahiki zitachukuliwa  Kiganja amesema, mpasuko huo pia umepelekea baadhi ya wanachama wanaoona hawaridhishwi na mwenendo mzima na pengine hata taratibu za suluhu zilizopo kuzikiuka na kuziona hazifai na kuamua kukimbilia mahakamani.Kiganja amesema, athari za kupeleka jambo hili mahakamani ni kubwa kwa vilabu na TFF kwa ujumla wake na kutokana na hali ilivyo BMT kama chombo pekee cha kisheria kilichopewa dhamana ya kusimamia michezo nchini hakiwezi kuvumilia ukiukwaji wa sheria unaoendelea ambao unaashiria kutoweka kwa amani katika tasnia ya michezo nchini.Amesema kuwa Baraza hilo limezingatia sheria yake na kanuni za msajiri namba 441, kanuni ya 11 kifungu kidogo cha (1-9) na kwamba atakayekiuka agizo hilo sheria itachukua mkondo wake.

0 comments:

Post a Comment