Sunday, October 16, 2016

Mashabiki wa SIMBA wamuweka kati shabiki wa YANGA



          Leo ligi kuu Tanzania bara iliendelea kwa baadhi ya viwanja macho na masikii ya mashabiki wa soka yalielekezwa katika  pambano la AZAM na YANGA pambano lililokuwa likionyeshwa  na chanel ya Azam two mojakwa moja toka uwanja wa uhuru  katika mtanange huo mashabiki wa Simba na wale wa Azam waliungana kuishabikia timu ya Azam kwa nguvu zote. Mchezo huo ulionekana kuwa wa kibabe uliotawaliwa na kadi kazaa  za njano na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu yoyote ilioweza kuona lango la mwenzake
          Baada ya mapumziko hayo upinzani wa maneno kwa mashabiki wa Azam na Yanga ukaanza, Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kilatimu ikifanya mashambulizi ya kushtukiza ila mpaka kipindi cha pili kinamalizika si Azam wala Yanga walioweza kuona lango la mwenzake baada ya  mpira kumalizika ndipo zogo lilinza kati ya Mashabiki wa Simba walio ongozwa na shabiki aliefahamika kwajina moja la MITHUNI huku upande wa mashabiki wa  Yanga waliongozwa na shabiki aliefahamika kwa jina moja la ADAMU ubishani huo uliendeea kwa kurushiana maneno huku mashabiki wa simba wakiwazomea mashabiki wa Yanga na kuwataka wasome alama za nyakati,  Shabiki wa yanga Adamu alionekana kutokuwa na raha kutokana na sare walioipata huku akiwaambia mashabiki wa Simba kuwa yeye ni Yanga damu kauli iliowapagawisha mashabiki wa Simba walioamua kumuweka kati shabiki huyo huku shabiki mmoja wa Simba MITHUNI alionekana kutoa fedha na kuagiza mabomba zaidi ya kumi ya sindano ili wamtoe damu yote nyekundu shabiki huyo kisha wampeleke hospitali ili awekewe damu ya njano kama ipo ili azihirishe kuwa yeye ni Yanga damu kitendo hicho kilimshitua shabiki hiyo wa Yanga na alipopata upenyo alijimasua kwa kukimbi toka eneo hilo

0 comments:

Post a Comment