Timu ya Simba imeonekana kuwa bora zaidi hasa kutokana na kutokuwa
na kikosi kimoja cha kwanza hii imejizihirisha katika mechi mbili
ilizocheza ambazo ni ile ya mbao fc na ile ya toto tofauti na meshi ya za
nyuma combination iliokuwa ikichezeshwa na iliozoeleka ni ile iliopachikwa jina la KIAMA
yaani Kichuya, Ajibu na Mavugo ila mechi ya Toto dhidi ya Simba walianza na
combination ambayo mashabiki wa timu hiyo tayari wameipachika jina la
IBM yaani Ibrahim, Blagnon pamoja na Mzamiru yasini huku Kichiya
akipewa majukumu ya kuilisha Combination hiyo.
Hata hivyo katika pambano hilo kati ya Simba na Toto ambapo simba iliibuka na ushindi wa goli tatu kwa bila Shiza Kichuya
alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Hamisi ndemla mabadiliko ambayo
yalizidi kuliweka lango la Toto katika wakati mgumu zaidi na
kujizihirisha kuwa licha ya Combination ya KIAMA hata IBM nayo inamakali
sawa na combination tulio izoea kwa jina la KIAMA hivyo laiti Sheria za
Soka zingekuwa zinaruhusu basi Simba inayo uwezo wa kucheza mechi mbili
kwa wakati mmoja na ikaibuka na ushindi mnono kwani makipa wapo wa
uhakika alikadhalika viungo pamoja na mabeki.
0 comments:
Post a Comment