Sunday, October 30, 2016

Ukuta uliowashinda Yanga na Azam kuupanda Je Simba itauweza kuupanda?



          Baada ya timu ya Simba kuichapa Mwadui FC kwa jumla ya magoli 3_0 katika muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara alimaarufu kwa jina la Vodacom sasa wekundu hao wa Msimbazi watakutana na timu kisiki ya Stendi United  alimaarufu chama la wana siku ya juma tano ya tarehe 02/10/2016 huko Mkoani Shinyanga timu hiyo ambayo katika rekodi yake ya ligi hiyo tayari imesha zirarua timu mbili vigogo vya ligi kuu Yanga na Azam katika uwanja wake wa nyumbani.

       Macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini yanasubi mtanange huo kwa hamu zaidi hasa ukizingatia timu ya Simba bado haijapoteza mchezo wowote kati ya michezo 12 iliochuka dimbani haliyakuwa Stendi nayo inataka kujiwekea rekodi ya kuziazibu timu kongwe ktk uwanja wake wa nyumbani. Mchezo huo unaonekana kuwa wa presha zaidi hasa kwa mashabiki wa timu zote huku mashabiki wa Yanga na wale wa Azam wakiomba Simba kupoteza mchezo huo ili kuwe na tofauti ndogo ya point kwani mpaka sasa Simba ndio wanaongoza ligi kwa kujikusanyia point 32 baada ya kushuka dimbani mara 12 wakifuatiwa na mahasimu wao Yanga wenye point 24 huku wakiwa wameshika dimbani Mara 11.

      Yanga wanatarajia kushuka dimbani leo tarehe 30/10/2016 kucheza mchezo wake wa 12 katika uwanja wa Uhuru wakiwakaribisha Mbao Fc timu ambayo imeonekana kuwa na upinzani wahali ya juu pindi inapo kumbana na timu kongwe za Simba na Yanga ktk mechi ya Simba na Mbao Simba iliibuka na ushindi wa goli moja kwa bila goli lililofungwa dakika za lala salama na Mzamiru yassini. Musoma24hrs inazitakia kila la heri timu zote zitakazo shuka dimbani siku ya leo tarehe 30/10/2016 na kwakua soka ni mchezo wa amani hivyo timu zote zicheze kwa nidhamu alikadhalika waamuzi nao kuchezesha mechi hizo kwa kufuata sheria za soka.

0 comments:

Post a Comment